Saturday, January 22, 2011

TANZANIA IKO TAABANI KAMA ILIVYOKUWA MELI MV BUKOBA 21 MAY, 2006

Na Aloyce Kalunde
Inaskitisha sana pale rais anaporuhusu ndani ya nchi ya Kambalage yaibuke matabaka ya u-dini, ukabila, na u-kanda, hii ni hatari sana kwa taifa letu na inapaswa kukomeshwa mapema, vinginevyo damu itamwagika katika kila kona na umaskini utatutembelea mara dufu zaidi ya ilivyo sasa.

Ushahidi wangu ni huu ndogo sana ambao nimeufanya kautoka eneo dogo hasa kwenye chuo kimoja cha serikali kijulikanacho kwa jina la University of Dodoma (UDOM) ambapo wafanyakazi wake wote walioshikilia nafasi za juu zaidi chuoni hapo ni waislamu (muslims), ispokuwa mkuu wa chuo tu ambaye ni mkatoliki. Hapa swali ni je, mchakato uliotumika kuwapata watumishi hao ulitumia sifa zipi? Na ili mtu aajiliwe UDOM kwenye wadhifa wa juu anatakiwa kuwa na sifa zipi?

Kwamujibu wa wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma hasa ngazi za juu, nimeptwa wasiwasi kwenye Nyanja zifuatazo: mabalozi wanaoteuluwa na rais kwenda nchi za nje, wabunge wa kuteuliwa wanaoingia Bungeni kwa viti maalumu, wakuu wa majeshi kama vile Jeshi la wananchi, jeshi la kujenga taifa na Polisi. Inawezekana kabisa kuwa kupanda cheo ni hadi uwe muislam au utoe rushwa ama uwe motto wa kigogo hapa nchini.

Haya ndiyo mambo yanayoifanya serikali ya rais Kikwete ionekane kuwa na ubabaishaji wa hali ya juu sana. Ni kwasababu watu wanapewa kazi kwa kujuana, kuwa dini moja au urafiki. Ingekuwa kila mtu anaingia kwa sifa zake kitaaluma migogora UDOM insingekuwa inatokea namna hii.

Ushahidi wangu kuwasilisha hisia za mshituko kuwa Tanzania tumeingiliwa na mdudu alaye zaidi ya kirusi kisababishacho ukimwi (UDINI) ni majina ambayo ni haya hapa:

Mh.B.W.Mkapa – Councilor, Dr. Mohamed bilal (vice president of Tanzania) - chairman., Prof. Idris Kikula - vice councilor, Prof. Shaban Mlacha - deputy vice councilor in planning, finance and administration (DVC PFA), Prof. Ludovick Kinabo - deputy vice councilor in academic, research and consultancy (DVC ARC), Prof. Kosaki - Principal collage of education, Mr. Manongi - Dean of students.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa serikali, dini na waumini hata wasio waumini kuwa, upendeleo wa nyadhifa haukwepeki, lakini inapotokea inzidi kiasi hiki watu lazima tushituke. Ni lazima tuhoji sasa kuwa si ajabu hata kupatikana kwa kura za mheshimiwa kikwete inawezekana zinau-dini ndani yake. Upendeleo huu ukiendelea utasababisha mpasuko wa wananchi kidini, itikadi, ukabikabila, ukanda na hata rangi. Na ikitokea hivyo ujue damu inakaribia kumwagika. Haya yalitokea Congo, Rwanda 1994, Brundi, Lebanon, Uudan, Sieralaeon, na kwingineko.

Tuweni makini na huu mpasuko, siwezi kusita kusema kuwa rais kikwete nchi imekushinda kuiongoza, na siyo mimi tu bali hata wananchi waliokupigia kura mwnzo walishituka kuwa uliwadanganya kuwa maisha bora kwa kila mtanzania, na ndoyo maana kura zimepungua sana za ushindi ukilinganisha na ulivyoshinda ktk uchaguzi wa 2005.

Tukianza kubaguana, je hii nchi itajengwa na watu gain?

Source: prospectus of UDOM 2010-2011.

No comments:

Post a Comment