Friday, January 14, 2011

MAPINDUZI HALISI HAYAJI KAMA USINGIZI

Mabadiliko ya namna yoyote ile hasa kisiasa popote pale daima hayaji kama usingizi, ili mabadiliko yaje ni hadi watu wachache wakubali kumwaga damu kwa manufaa ya wengi.
Mke wa Dr.SLAA kajeruhiwa na polisi kwenye mkutano huko Arusha tarehe 5januari,2011.

Ni maandamano ya amani huko Arusha yaliyosababisha mashujaa, na wapenzi wa CHADEMA wawili wauliwe na polisi.

Ifahamike wazi kuwa POLISI ndio chanzo cha vulugu hapa nchini, kwasababu kama wasingekuwa chanzo cha vurugu kwanini Mkusanyiko wa kuwaombea na kuwaaga Marehemu walioliwa na Polisi siku ya maandamano, uliokusanya maelfu ya wananchi waliojitokeza, mbona hawakufanya shali yoyote? na kwanini? hapakutokea ajari zozote pamoja na trafiki kutokuonekana kabisa eneo la tukio. jibu linakuja kuwa vyombo vya dola tulivyovipa imani kubwa kulinda usalama wa raia na mali zao kumbe ndivyo vinahusika kwa 100% kufanya uhalifu. Angalizo hapa ni kwamba, Roho za watanzania na damu inayomwagika bila hatia itawadai siku ya mwisho. na itafika hatua watanzania watachoka, watachoshwa na bugudha mnazowafanyia, watasema inatosha, na wakisema inatosha sikuhiyo patakuwa ni kivumbi.

Mwisho nahitimisha kwa kusema kuwa, kunakila sababu ya wewe IGP Said Mwema kujihuzuru pamoja na waziri wa Mambo ya ndani, ili kunusuru roho za watanzania.

No comments:

Post a Comment